Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii

Kagame akubali kukutana na Tshisekedi, upinzani Burundi wamfukuza rais wake chamani, Ousmane Sonko aachiwa kule Senegal...

Informações:

Synopsis

Kwenye Makala ya wiki hii tunaangazia hatua ya Rais Kagame kukubali kukutana na mwenzake wa DRC Tshisekedi, pia tutaangalia alivyofukuzwa chamani kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwassa, lakini vilevile kilichojadiliwa katika mkutano kati ya marais wa Kenya, Tanzania na Uganda. Tutatupia jicho hali ya kibinadamu nchini Sudan, lakini pia siasa za Senegal baada ya kuachiwa kwa Ousmane Sonko, siku chache kabla ya uchaguzi wa Machi 24, kule Nigeria tutaangalia yanayojiri baada ya wanafunzi kutekwa na rais Tinubu kusema hawatatii agizo la watekaji la kutaka kulipwa ili kuwaachia wanafunzi hao.Pia hali kule Haiti baada ya waziri mkuu Ariel Henry kukubali kujiuzulu, Meli ya kwanza ya chakula cha msaada kutoka Cyprus kuwasili Gaza na pia siasa za Marekani baada ya rais Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump kushinda uteuzi katika vyama vyao.Niliyeshika usukani ni Jupiter Mayaka kwa niaba ya Ruben Lukumbuka ambaye yuko Pwani ya Kenya anakula upepo wa bahari. Kwa mengi zaidi bonyeza linki usikilize