Habari Za Un
Mradi wa IFAD wasaidia vijana Senegal kusalia nchini mwao, kulikoni?
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:04:07
- More information
Informações:
Synopsis
Mradi wa uitwao Agri-Jeunes uliozinduliwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo, IFAD ili kusaidia raia wa Senegal kuondokana na umaskini, na janga la njaa, umewapatia vijana wa kiume na wa kike matumaini ya kusalia nchini mwao badala ya kuhamia ughaibuni. Mradi huu umewasaidia vijana hao kwa mafunzo ya kilimo, ufugaji kuku, uvuvi na stadi za kuendesha biashara ndogondogo.Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2024, makumi ya maelfu ya watu waligeukia wasafirishaji haramu wa binadamu kwa njia ya bahari ya Atlantiki kuelekea visiwa vya Kanari, lakini zaidi ya watu 5000 wamekufa wakijaribu kufika huko. Haya yote yakisababishwa na ukosefu wa ajira na kipato duni. Kupitia video iliyoandaliwa na IFAD, Bosco Cosmas amefuatilia Maisha ya vijana hao, na kutuandalia makala hii