Habari Za Un

Fahamu mbinu itumiwayo Afrika Kusini kukabili Virusi Vya Ukimwi

Informações:

Synopsis

Kuelekea ya Siku ya Kimataifa ya UKIMWI itakayoadhimishwa Jumapili hii, ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na UKIMWI (UNAIDS) iliyotolewa juzi Jumatano imeeleza kuwa dunia inaweza kufikia lengo lililokubaliwa la kukomesha UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030 lakini kwa sharti kwamba viongozi ni lazima walinde haki za binadamu za kila mtu anayeishi na Virusi Vya UKIMWI, VVU au aliyeko hatarini kuambukizwa. Anold Kayanda ameangazia mfano mzuri wa Afrika Kusini unaofahamika kama “Takuwani Riime”.