Habari Za Un

27 NOVEMBA 2024

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya na lishe katika nchi zinazokumbana na ukame. Makala tunakwenda Ureno na mashinani nchini Sudan, kulikoni?Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, amesema amestushwa na kusikitishwa na kifo cha aliyetarajiwa kushika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Faustine Engelbert Ndungulile kutoka nchini Tanzania.Awamu ya pili ya mradi wa kuboresha lishe, SUN II nchini Zambia umewezesha wakulima kupanda mazao yanayohimili ukame na vile vile kukabiliana na viwavi jeshi kwa kutumia mbinu za asili, mradi uliotekelezwa na shirika la Umoja la kuhudumia watoto, UNICEF ili wakulima wasikumbwe na njaa wakati huu ambapo ukame umetikisa nchi za kusini mwa Afrika.Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu limekunja jamvi leo huko Cascais, Ureno ambako sambamba na jukwaa hilo, pia vijana kutoka makundi 150 duniani walikusanyika katika jukwaa lao wakiwemo watengeneza filamu chipukizi ambao kupitia filamu wanaeleza mambo kadha ya ulimwengu k