Habari Za Un
UN: Mwanamke au msichana mmoja aliuawa kila baada ya dakika 10 na mwenzi au ndugu 2023
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:03:13
- More information
Informações:
Synopsis
Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza? Maudhui ya siku hii yanasema “Hakuna kisingizio” cha ukatili dhidi ya wanawake lama alioushuhudia Ester manusura kutoka Uganda, ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifanyiwa ukatili na mpenzi wake anaema “Nilikuwa na umri wa miaka 15 aliponioa naye alikuwa na miaka 28wakati mwingine alikuwa akinivua nguo zote na kunilazimisha kukaa kwenye varandana nilikuwa nikichelewa kurudi ananitandika nje nyumba kila mtu kushuhudia Nilikuwa katika hali mbaya ya uchungu Mkubwa na kuvuja damu.”maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na ripoti iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la masuala ya wanawake, UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mata