Habari Za Un

12 DESEMBA 2024

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ikiangazia wanawake na wasichana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambapo ukatili wa kingono ni jinamizi linalowakumba kila uchao kutokana na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno MIDABWADA.Leo si siku ya kimataifa ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba mudhui “Huduma za afya kwa wote ni jukumu la serikali” yakisisitiza kwamba Uwekezaji katika huduma za afya kwa wote UHC, unaimarisha usawa na uwiano wa kijamii na pia unanufaisha uchumi wa taifa kwa kuboresha afya na ustawi, kuongeza ushiriki wa wafanyikazi na tija, na kujenga mnepo kwa watu, familia na jamii.Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syri Geir O. Pedersen leo amesema “Picha kutoka kwenye magereza ya Sednaya na vituo vingine vya kizuizini nchini Syria vinadhihirisha unyama na ukatili usiofikirika ambao Wasyria wamevumilia na umekuwa ukiripotiwa kwa miaka mingi.”Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko z