Habari Za Un

11 DESEMBA 2024

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO inayohusu malaria, na juhudi za UNICEF na wadau wake nchini Rwanda za kusaidia watoto waliozaliwa na ulemavu kuweza kutembea. Makala tunakupeleka nchini Yemen na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Takwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO na hivyo juhudi zaidi zahitajika kuutokomeza.Nchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Uswisi na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Yemen kusikia yaliyojiri baada ya ndoto za vijana kuelekea Saudi Arabia kuishia Yemen.Na mashinani mashinani hivi majuzi d