Habari Za Un
09 DESEMBA 2024
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:59
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Syria, na kampeni ya chanjo ya polio huko Pokot nchini Kenya. Makala tunasalia huko huko DRC na mashinani tnakwenda nchini Msumbiji, kulikoni?Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya hivi karibuni wamezindua kampeni ya chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa.Makala tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza mama ambaye alipatiwa ujauzito na mlinda amani wa Umoja wa Mataifa na kisha kujifungua mtoto ambaye anasimulia kadhia ya kutomf