Habari Za Un

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:51:49
  • More information

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • 26 NOVEMBA 2024

    26/11/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakletea mada kwa kina ambayo tunamskia mwanamke mjasiriamali kutoka visiwa vya Karibea St. Kitts na Neves akitumia fursa ya utamaduni wake mchanganyiko wa asili ya Visiwa hivyo na wa Kiswahili kujikwamua kiuchumi kupitia ubunifu wa mitindo na shughuli za mama lishe. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mgogoro Lebanon, Afya ya kinywa, na Ujumbe wa Katibu Mkuu kutoka Portugal akihutubia Jukwaa la 10 la Umoja wa Mataifa la Muungano wa Ustaarabu, (UNAOC). Mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza kumsikia muathirika wa vita ya Israel.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

  • Tanzania: FAO yawezesha ufugaji kuku bila kutumia dawa ili kuepusha UVIDA

    25/11/2024 Duration: 03min

    Nchini Tanzania wanufaika wa  mradi wa kudhibiti usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa, (AMR) au kwa lugha ya Kiswahili, (UVIDA) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi wamezungumzia manufaa ya ufugaji wa kuku bila kutumia dawa. Unaweza kujiuliza wanafuga vipi kuku bila kutumia dawa. Na je ni kwa nini wanafanya hivi. Je hawatumii dawa kabisa au wanafanya nini?Katika makala hii, mwandishi wa habari wa Redio washirika wetu Tanzania Kids Time ya mkoani Morogoro,mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, Hamad Rashid, amezungumza na wanufaika hao  ambao pia walipata nafasi ya kuonesha shamba darasa la ufugaji kuku bila ya kutumia dawa kupitia hafla iliyoratibiwa na FAO katika shule ya sekondari Kihonda, Manispaa ya Morogoro, ikienda sambamba na Wiki ya utoaji elimu kuhusu UVIDA  ambayo hufanyika duniani kote kila ifikapo tarehe 18 hadi 24 mwezi Novemba. Kwako Hamad.

  • MONUSCO yaitikia ombi la Meya wa Beni, Kivu Kaskazini DRC

    25/11/2024 Duration: 01min

    Kiu cha Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, cha kuona daraja linalounganisha barabara muhimu linakarabatiwa kilipata jawabu baada ya ombi lake kwa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kuchukua hatua ambayo pia inawezesha doria za ulinzi wa raia mjini humo. Maelezo kamili anayo George Musubao kutoka Beni, katika taarifa hii tuliyoitoa kwenye ukurasa wa X wa MONUSCO. 

  • 25 NOVEMBA 2024

    25/11/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, na Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC la kukarabati daraja linalounganisha barabara muhimu. Makala tunakwenda nchini Tanznaia na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza?Kiu cha Meya wa mji wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, cha kuona daraja linalounganisha barabara muhimu linakarabatiwa kilipata jawabu baada ya ombi lake kwa Ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kuchukua hatua ambayo pia inawezesha doria za ulinzi wa raia mjini humo.Makala inatupeleka Tanzania kwake Hamad Rashid wa redio washirika Kidstime FM ya mkoani Morogoro

  • UN: Mwanamke au msichana mmoja aliuawa kila baada ya dakika 10 na mwenzi au ndugu 2023

    25/11/2024 Duration: 03min

    Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake, Je wajua kwamba wanawake na wasichana 140 walifariki dunia kila siku duniani kote mwaka 2023 wakiwa mikononi mwa wapenzi wao au ndugu wa karibu, ikimaanisha kuwa mwanmake mmoja anauawa katika kila dakika 10. Na zaidi ya yote bara la Afrika linaongoza? Maudhui ya siku hii yanasema “Hakuna kisingizio” cha ukatili dhidi ya wanawake lama alioushuhudia Ester manusura kutoka Uganda, ambaye kwa miaka mingi amekuwa akifanyiwa ukatili na mpenzi wake anaema “Nilikuwa na umri wa miaka 15 aliponioa naye alikuwa na miaka 28wakati mwingine alikuwa akinivua nguo zote na kunilazimisha kukaa kwenye varandana nilikuwa nikichelewa kurudi ananitandika nje nyumba kila mtu kushuhudia Nilikuwa katika hali mbaya ya uchungu Mkubwa na kuvuja damu.”maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na ripoti iliyotolewa leo jijini New York, Marekani na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la masuala ya wanawake, UN Women na Ofisi ya Umoja wa Mata

  • Vijana wajumuishwe kwenye majadiliano ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi - Nasra

    22/11/2024 Duration: 03min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania umewajumuisha watoto kwenye harakati za kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Huko Baku nchini Azerbaijan kunakotamatika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 tunamsikia Nasra Abdallah, mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania akizungumzia kilichompeleka, anachoondoka nacho na ujumbe wake kwa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

  • Kuna mkwamo kwenye mkutano wa COP29 huku mapendekezo mapya yakitaka nchi tajiri kuzilipa masikini dola bilioni 250 kwa mwaka

    22/11/2024 Duration: 02min

    Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea. Hakika vuta nikuvute bado inaendelea hata sasa washiriki wako mezani kwakikuna vichwa na kujadili mapendekezo mapya. Mkwamo huo umetokana na kushindwa kuafikiana katika masuala kadhaa kubwa likiwa ufadhili wa  mabadiliko ya tabianchi na hususasn kuhusu ni kiasi gani cha fedha nchi zinazoendelea zinapaswa kupokea kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2030 na wapi fedha hizo za ufadhili zitatoka.Nchi zinazoendelea zinataka kulipwa dola trilioni 1.3 kwa mwaka lakini hilo halijaafikiwa na mapendekezo mapya yaliyowasilishwa na raia wa mkataba huo wa UNFCCC yanaonyesha tofauti kubwa na safari ndefu ya kufikia muafaka.Kwa mujibu wa mapendekezo hayo mapya yaliyowasil

  • 22 NOVEMBA 2024

    22/11/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia majadiliano huko Baku Azerbaijan kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi, na kazi za walinda amani kutoka Tanzania TANZBATT-11 huko DRC. Makala inaturejesha kataika mkutano wa COP29 na mashinani inatupeleka Namibia, kulikoni?Majadiliano ya mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 yamekumbwa na mkwamo huko Baku Azerbaijana muafaka haujapatikana. Majadiliano hayo yaliyotarajiwa kukunja jamvi leo sasa yanaendelea kwa kuwekwa mezani mapendekezo mapya kuhusu ufadhili wa mabadiliko ya tabianchi hasa kwa matifa yanayoendelea.Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto.Makala ina

  • Mafunzo ya walinda amani kutoka Tanzania huko Beni yajengea uwezo walimu kusaidiana na watoto

    22/11/2024 Duration: 02min

    Umoja wa Mataifa unasema kwamba vita mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefanya taifa hilo kuwa pahala hatari zaidi duniani kwa watoto kuishi, kutokana na mateso ya kimwili na kisaikolojia wanayoyapitia. Kwa kutambua hilo walinda amani wanawake wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa UN nchini humo, MONUSCO wamechukua hatua kuona watoto wanaishi kama watoto. Video ya MONUSCO ikianza na walinda amani wakijongea kwa jamii, Kapteni Noella Nyaisanga kiongozi wa kikundi hicho cha wanawake cha kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania kwenye MONUSCO, TANZBATT-11 anaeleza jinsi kikundi chao kinavyosogea kwa jamii na hasa watoto ili kutatua changamoto zinazowakabili kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi kwenye eneo hili la Beni, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Anafafanua zaidi lengo lao.Lengo ni kujenga uaminifu kwa raia ambao tunawalinda. Kwa hiyo tukaamua kuandaa masomo shuleni, ambayo yataweza kuwaimarisha wao, kuwasaidia tatizo la kuwa

  • Jinsi usawa wa kijinsia na rika katika umiliki wa ardhi unavyochochea ukulima na uhakika wa chakula Kenya

    21/11/2024 Duration: 05min

    Mpango wa Usimamizi wa Ardhi (Land Governance program) uliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi (land reforms) katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi na umeimarisha usimamizi wa ardhi kwa ajili ya maisha bora na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika kaunti zote zinazotekeleza. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO, Cecily Kariuki anaeleza matokeo yake.Mpango wa Usimamizi wa Ardhi (Land Governance program) uuliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi (land reforms) katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi k

  • 21 NOVEMBA 2024

    21/11/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kushuhudia jinsi mpango wa Usimamizi wa Ardhi uliopatiwa wa "kusaidia jamii kufikia Ajenda 2030” ambao FAO imetekeleza kwa kaunti kadhaa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Hague kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ICC ambayo leo imetoa kibali cha kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa zamani wa ulinzi Yoav Galant  na kiongozi wa kundi la kipalestina la Hamas Mohamed Diab Ibrahim al-Masri alimaarufu kama  kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhaifu wa vita ulitendeka wakati wa vita inayoendelea baina ya Israel na Hamas.Mjini  Baku nchini Azerbaijan mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachanama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabainchi COP29 unaelekea ukingoni  na leo ukijikita na masuala ya kijinsia na mabadiliko ya tabianchi. Miongoni mwa waliozungumzia changamoto ya tabianchi kwa wanawake ni  Jemimah Njuki, mkuu wa

  • COP29 Georgina Magesa: Watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama

    20/11/2024 Duration: 04min

    Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 unaoendelea huko Baku Azerbaijan umeleta pia watoto na vijana wanaharakati wa mazingiria kutoka kote ulimwenguni na kuwapatia fursa kuketi katika meza moja na viongozi ili kuhakikisha mustakabali wao umewekwa katika ajenda ya mkataba huo. Jukumu lao kama wachechemuzi wa mabadiliko chanya na hitaji la mazungumzo na ushirikiano kati ya vizazi lilitambuliwa rasmi katika matokeo ya Mkutano wa Zama Zijazo, SOTF mnamo Septemba 2024.Georgina Magesa, msichana mwenye umri wa miaka tisa na mwanaharakati wa mazingira, ambaye amewakilisha watoto wenzake kutoka Tanzania katika Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan. Anatoa ujumbe mahsusi akianza kwa kusistiza kuwa watoto pia wana mchango katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi.“Watoto wenzangu duniani kote, nyie pia mnaweza kuleta mabadiliko chanya. Anza na hatua ndogo p

  • 20 NOVEMBA 2024

    20/11/2024 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti siku ya watoto duniani, na kwa kutambua siku hii tunamulika mikutano yote yanayoendelea kwa ajili ya haki za watoto na vijana, ambao wametoa ujumbe wao kutoka Baku nchini Azerbaijan na Denmark wakiwakilisha nchi zao.Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao.Kama ulivyosikia katika taarifa yetu ya kwanza leo ni siku ya watoto duniani ikirejelea tarehe 20 Novemba mwaka 1954 kwa mara ya kwanza kabisa ilipoanzishwa na Umoja wa Mataifa kusongesha umoja na kujitambua miongoni mwa watoto duniani..Makala ikiwa leo ni siku ya watoto duniani, tunakupeleka Baku Azerbaijan katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi

  • UNICEF - Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto duniani yafanyika Denmark

    20/11/2024 Duration: 01min

    Leo ikiwa ni siku ya watoto duniani ikirejelea tarehe 20 Novemba mwaka 1954 kwa mara ya kwanza kabisa ilipoanzishwa na Umoja wa Mataifa ili kusongesha umoja na kujitambua miongoni mwa watoto duniani. Kisha siku hii ikaongezwa nguvu na Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto duniani mwaka 1959 na hatimaye mwaka 1989 Baraza hilo lililopitisha Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto, CRC. Mkataba unatambua haki kuu nne za msingi za mtoto: Kuishi, Kuendelezwa, Kulindwa na Kushirikishwa. Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limefanya maadhimisho ya kimataifa huko Copenhagen Denmark, na Madina Jubilate, Mchechemu wa UNICEF Tanzania kwa Tabianchi anaelezea alivyoshiriki.

  • Waraka kutoka kwa watoto: Kwenu watu wazima, kwa nini mnauruhusu mustakbali wetu kuwekwa rehani?

    20/11/2024 Duration: 02min

    Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao. Hao ni baadhi tu ya makumi ya watoto walioandika barua , hawa ni kutoka Gaza, Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC ambao walishika kalamu na karatasi kufikisha ujumbe wao kwa watu wazima wa dunia ya sasa iliyoghubikwa na changamoto lukuki zinazoweka rehani mustakbali wao.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF ya “Hali ya watoto duniani mwaka 2024: Mustakabali wa Utoto katika Ulimwengu Unaobadilika,” iliyotolewa leo sanjari na maadhimisho ya siku hii kuna masuala matatu makubwa ya kimataifa yatakatoathiri maisha ya watoto ifikapo 2050 na kuendelea. Mosi ni mabadiliko katika idadi ya watu, pili janga la mabadiliko ya tabianchi na mi

  • 19 NOVEMBA 2024

    19/11/2024 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku nchini Azerbaijan kwenye mkutano wa COP29. Miongoni mwa mambo yanayopigiwa chepuo ni madini ya kimkakati yanayoelezwa kuwa ni jawabu la nishati chafuzi kwa mazingira na tunapata ufafanuzi kutoka kwa Adam Anthony, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali nchini Tanzania.Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewasihi viongozi wa kundi la nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G20 wanaokutana huko Rio De Janeiro, Brazil kuwaagiza mawaziri na washawishi wao huko COP29 wahakikishe wanakubaliana juu ya lengo jipya na kubwa la mwaka huu la ufadhili kwa tabianchi nchi. Guterres amesema sambamba na hilo ni vema kukabiliana na taarifa potofu kuhusu tabianchi.Huko Kusini mwa Lebanon, walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha Mpito nchini humo, UNIFIL, wameshuhudia uharibifu mkubwa wa kutisha kwenye vijiji vilivyoko sambamba na eneo      la kati ya Israeli na Lebanon lisilopaswa kuwa na map

  • Uganda inaendelea na mapambano ya kutunza wakimbizi licha ya changamoto za kifedha

    18/11/2024 Duration: 05min

    Kwa miongo kadhaa sasa mfumo wa Uganda wa kuwaweka wakimbizi kwenye makazi badala ya kambi, umesaidia kujengea mnepo wakimbizi na hivyo wanaweza kujitegemea. Wakimbizi wanapata huduma za msingi kama vile hata ardhi ya kulima na kufugia mifugo ili kujipatia kipato. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Selina Jerobon amefuatilia hadithi ya mama mkimbizi kutoka Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye baada ya kupitia machungu na kukimbilia nchini Uganda sasa ameanza kuwa na matumaini ingawa ukata unatishia huduma kama alivyojionea mwenyewe Fillipo Grandi, Kamishna Mkuu wa shirika hilo.

  • Vijana wafurahia stadi za kuondokana na umaskini Sudan Kusini

    18/11/2024 Duration: 01min

    Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Shamrashamra zilitawala wakati vijana 61, wakiwemo wasichana 41 na wavulana 20 walipohitimu mafunzo ya ufundi stadi yenye lengo la kuwaondoa katika umaskini na pia kuwaepusha kutumikishwa katika mzozo unaoendelea nchini humo tangu Desemba 2013.Walifundishwa urembo wa nywele, kutengeneza sabuni, halikadhalika ushoni, mafunzo yaliyofadhiliwa na UNMISS na kutolewa na shirika la kiraia Star Trust Organization, linalohusika na kupunguza ghasia kwenye jamii kwa kuwajegena vijana uwezo.Miongoni mwao ni Suzan James, mama wa watoto wawili aliyejifunza urembo wa nywele na akiwa anamhudumia mteja wakati wa mafunzo anasema.“Ninashukuru mno, kwa sababu nimejifunza mambo mengi ambayo awali sikuyafahamu, lakini sasa ninaweza kufanya. Inanisaidia sana, na ninajivunia na nina furaha.

  • 18 NOVEMBA 2024

    18/11/2024 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa ndani nchini Haiti, na mafunzo ya stadi za kujikimu kimaishwa kwa vijana Tambura Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Katika makala Selina Jerobon kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anakupeleka Uganda kuona harakati za wakimbizi

  • IOM: Zaidi ya watu 20,000 wamefuriushwa ndani ya siku 4 Haiti kutokana na machafuko ya magenge ya uhalifu

    18/11/2024 Duration: 02min

    Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince (POTOPRINSI) limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Kupitia taarifa iliyotolewa leo na IOM nmini Port-au-Prince asilimia kubwa ya watu hawa waliofurushwa makwao wametawanywa zaidi ya mara moja wakilazimika kukimbia na kuacha kila kitu walichokuwa nacho na shirikika hilo linasema kiwango hiki cha watu kutawanywa hakijashuhudiwa Haiti tangu Agost 2023.Shirika hilo linasema kufungwa kwa usafiri wa anga kufuatia shambulizi lililolenga ndege tatu za kibiashara mjini Port-au-Prince, kuzuia ufikiaji wa bandari kuu ya nchi hiyo, na barabara zisizo salama zinazodhibitiwa na makundi yenye silaha kumeliacha eneo la Katikati ya m

page 3 from 5